Mali za DECI zataifishwa

0
400

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam imekubali ombi la Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), – Biswalo Mganga la kutaifisha mali za kampuni iliyokua ikiendesha biashara ya upatu ya Development Enterpreneurship For Community Initiative (DECI).

DPP Mganga ameiambia TBC  kuwa mali hizo ni pamoja na zaidi ya Shilingi Bilioni 14, magari Kumi, nyumba Tano na viwanja vitano.

DPP Mganga alifungua ombi  hilo katika Mahakama Kuu Kanda Dar es salaam ikiwa ni takribani miaka Sita baada ya viongozi wa DECI kutiwa hatiani na Mahakama ya  Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam katika kesi ya jinai namba 109 ya mwaka 2009 kwa kosa la kuendesha biashara ya upatu kinyume cha sheria.