Makongoro: Mwalimu alitaka kung’atuka mwaka 1980

0
230

Mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Makongoro Nyerere amesema, yeye alikuwa akizungumza na Mwalimu na walikubaliana ataachia madaraka ya Urasi mwaka 1980 lakini ikashindikana.

Makongoro ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara amesema, baada ya mazungumzo na mwalimu walijitokeza wakina mama waliomshawishi Mwalimu aendelee mpaka mwaka 1985.

Akitoa salamu za familia katika Mdahalo wa Kitaifa wa Kuadhimisha Miaka 100 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa uliofanyika Kibaha, Mkoani Pwani, Makongoro amesema mwalimu aliwapenda sana wakina mama ndio maana aliwasikiliza na kuendelea na uongozi wa nchi licha ya kutaka kung’atuka mwaka 1980.