Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda ametoa siku tano kwa
wakandarasi waliopewa mikataba ya ujenzi wa miradi mbalimbali hususanbarabara jijini Dar Es Salaam kukamilisha miradi hiyo ili kuondoa adhaya huduma ya usafiri kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam, Makonda
amezionya mamlaka zinazotoa zabuni kwa kandarasi zisizotekeleza miradi kwa wakati.
Katika hatua nyingine Makonda amewapongeza wakazi wa jiji la Dar Es
Salaam kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji wa
serikali za mitaa na kuwataka kujitokeza katika uchaguzi ili kuwa na
viongozi watakaosimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.