Makonda ataka kiandikwe kitabu kutambua kazi za Rais Magufuli

0
177

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, – Paul Makonda amemuomba Rais John Magufuli kama ataridhia, kiandikwe kitabu kitakachomtambua kama Mwanamapinduzi wa uchumi katika nchi yake ndani ya Bara la Afrika.

Akitoa salamu za Wakazi wa mkoa wa Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Pipe Industries Company Limited, Makonda amesema kuwa mambo yaliyofanywa na Rais Magufuli ni makubwa katika kipindi kifupi.

“Leo nina furaha sana, na kwa kweli furaha yangu ni kuona Mapinduzi yanayofanywa na wewe yanalenga kuwasaidia Watanzania, na huu ni uzalendo wa hali ya juu sana”, amesema Makonda.

Kuhusu ujenzi wa kiwanda hicho, kinachotengeneza mabomba ya maji na mabomba ya kusafirishia gesi na mafuta, Makonda amesema kuwa, kitasaidia kuongeza ajira na kukuza uchumi wa Taifa.