Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,-Paul Makonda leo amemtembelea Ashraf Hamza, ambaye alimsaidia kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Ashraf alikua na uvimbe katika eneo la uso wake na taarifa zake kusambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa anahitaji msaada wa upasuaji.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Makonda ametoa wito kwa Watanzania wote kuwa na utamaduni wa kukata bima za afya ili ziweze kuwasaidia pindi wanapopatwa magonjwa mbalimbali.