Makinikia yanayosafirishwa yameuzwa

0
205

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa, makinikia yote yanayosafirishwa yamefuata taratibu na hakuna makinikia yanayouzwa bila kulipiwa kwanza.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa ufafanuzi huo Bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, wakati akijibu swali la Mbunge wa Msalala, -Iddi Kassim Idd.

“Makontena yote yanayosafirishwa hivi sasa, tayari yameshauzwa na kulipiwa na fedha iko kwenye akaunti zetu, hapo yako chini ya mnunuzi na yeye yuko huru kuyapeleka anakotaka,”amefafanua Waziri Mkuu Majaliwa.
 
Mbunge huyo wa Msalala alitaka kujua Serikali inatoa kauli gani juu ya kontena zilizoshuhudiwa zikisafirishwa kupitia barabara ya Bulyanhulu-Kahama na bandari ya Dar es salaam licha ya kuwa ilishazuia makinikia kusafirishwa nje ya nchi.
 
Waziri Mkuu Majaliwa amekiri kwamba Serikali ilishazuia usafirishaji wa makinikia kwenda nje ya nchi katika kipindi cha mwaka 2017/2018 na kwamba zaidi ya kontena 300 zilizuiwa bandarini kwa sababu wahusika hawakufuata utaratibu na kulikuwa na udanganyifu.