Makatibu Tawala na Maafisa Tarafa watakiwa kuzungumza na wananchi

0
556

Rais John Magufuli amewaagiza Makatibu Tawala wa Wilaya zote na Maafisa Tarafa wa Tarafa zote hapa nchini hao kujenga utaratibu wa kuwatembelea, kuwasikiliza na kutatua kero na migogoro mbalimbali inayowakabili wananchi pamoja na kuchukua hatua pale ambao mambo hayaendi sawa.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo alipokutana na maafisa hao Ikulu Jijini DSM.