Makanjanja mwisho Disemba 2021, Waandishi wa habari watakiwa kujiendeleza

0
261

Waziri Wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe amesisitiza kuwa itakapofika Disemba 2021 ndio mwisho wa waandishi wa habari wasiokua na elimu kuanzia ngazi ya stashahada kufanya kazi hiyo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.

Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt Rioba akizungumza mbele ya Waziri na Naibu waziri wa HUSM

Dkt Mwakyembe ametoa kauli hiyo mkoani Singida alipokua anazungumza na wadau wa tasnia ya habari ambapo amewataka waandishi wa habari kutambua kuwa ikifika mwaka 2022 wale ambao watakuwa hawajakidhi vigezo kulingana na Sheria hiyo watakua wamejiondoa rasmi katika tasnia hiyo.

Waziri Mwakyembe akipata ufafanuzi kutoka kwa Mhandisi wa TBC Upendo Mbele

Aidha Waziri Mwakyembe ametembelea eneo la mitambo ya kuimarisha usikivu wa Shirika la Utangazaji TBC lililopo Mikumbi mkoani hapo na kusema kuwa Serikali inaendelea kuimarisha usikivu wa Shirika hilo ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 70