Makamu wa Rais wa Marekani kuwasili leo

0
156

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris anatarajiwa kuwasili nchini saa nne usiku hii leo, akitokea nchini Ghana.

Akiwa hapa nchini kwa ziara yake ya Kiserikali ya siku tatu, Kamala atakuwa na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan, mazungumzo yatakayofanyika hapo kesho Machi 30, 2023.

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) litakuletea matangazo Mbashara ya ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani kuanzia atakapowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mkoani Dar es Salaam.

Endelea kutufuatilia kupitia TBC1, TBC Taifa na mitandao ya kijamii ya TBCOnline