Makamu wa Rais atembelea Hospitali ya Uhuru

0
151

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akipata maelezo kuhusu maendeleo na changamoto mbalimbali zinazoikabili hospitali ya Uhuru iliyopo jijini Dodoma, kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Pius Kagoma, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo leo Aprili 26, 2021.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akizungumza na kusikiliza changamoto mbalimbali kutoka kwa Watendaji wa hospitali ya Uhuru iliyopo jijini Dodoma, alipofanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo leo Aprili 26, 2021.