Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke ambapo pamoja na mambo mengine balozi huyo amempa taarifa Makamu wa Rais juu ya ziara ya Mwanamfalme William wa Uingereza atakayewasili nchini wiki ijayo kwa ziara yake ya siku tatu.
Ziara ya Mwanamfalme William nchini ina lengo la kujifunza mambo ya uhifadhi wa wanyamapori kama sehemu ya maandalizi ya mkutano wa dunia unaohusu masuala ya uhifadhi wa wanyamapori utakaofanyika jijini London nchini Uingereza mwezi Oktoba mwaka huu.
Balozi Cooke pia amemjulisha Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yaliyofikiwa kwenye mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa nchi za Jumuiya ya Commonwealth uliofanyika mwezi aprili mwaka huu jijini London.