Makamu wa Rais aagiza kusimamishwa kazi Mkurugenzi Nanyumbu

0
339

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amefanya ziara ya kushtukiza katika stendi ya mabasi ya Mangaka iliyopo wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.

Katika ziara hiyo ameeleza kukasirishwa na uongozi wa wilaya kufanya upotevu mkubwa wa fedha usiolingana na matokeo ya ujenzi wa mradi huo. Ujenzi wa majengo ya stendi hiyo umetumia shilingi bilioni 2.2 kiasi ambacho amesema hakilingani na ujenzi huo.

https://www.instagram.com/tv/CRuCIjhFJHq/?utm_source=ig_web_copy_link

Amemuagiza Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu, Hamis Dambaya ili kupisha uchunguzi.

Amesema viongozi hawana budi kusimamia fedha za serikali zinazopelekwa katika maeneo yao ili kuwaletea wananchi maendeleo.