Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amewavua madaraka makamamanda wa polisi wa watatu kwa tuhuma za kutotekeleza maagizo ya viongozi na kuamuagiza katibu mkuu wizara ya hiyo kuunda tume itayochunguza tuhuma za vitendo na mianya ya rushwa katika jeshi hilo husuusani katika kikosi cha usalama barabarani ili kuchukua hatua.
Waziri Kangi Lugola ametoa uamuzi huo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari sambamba na kumtaka kamanda wa kikosi cha usalama barabarani kujitathmini kama anafaa kuendelea na nafasi hiyo akianza na suala la tume.
Makamanda hao ni pamoja na Salum Hamduni (Ilala),Emmanuel Lukula (Temeke) na Ramadhan Ngazi(Arusha).
Waziri amesema pia makamanda hao wa polisi wa mikoa mitatu wamekuwa wakishindwa kufanya majukumu na maagizo ya serikali katika utendaji wao.
Pi waziri Lugola amepiga marufuku kwa kikosi cha usalama barabarani kubambikiza makosa mengi kwa madereva na kutoza faini katika makosa hayo kinyume na sheria ya usalama barabani.