MAKALA YA UTUNZAJI MAZINGIRA YA ZIWA TANGANYIKA – BUHINGU KIGOMA

0
143

Karibu Buhingu moja kati ya vijiji 22 kando ya ziwa Tanganyika na ikolojia ya mahale wilayani Uvinza mkoani Kigoma, wakazi hawa wameunganisha nguvu na mtazamo mpya kwa kujenga jamii yenye kutumia raslimali ardhi na maji bila kuathiri urithi wa vizazi vijavyo,

Familia hapa zina afya na zinajikimu, huzalisha ziada kwa kutumia vyema mazingira yanayowazunguka huku wakizingatia matumizi bora ya ardhi kwa kufanya kilimo na uvuvi endelevu, kuzaa kwa nafasi bila kuathiri afya ya mama na mtoto

Wamefikia maendeleo haya  baada ya kuwezeshwa na  Shirika la kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Rasilimali, la ‘The Nature Consevancy’ yaani (T N C) pamoja na Shirika linalosimamia maswala ya Afya la Pathfinder International kwa kushirikiana na Serikali katika mradi wa Tuungane ambao umejikita katika kujengea uwezo jamii ili ziweze kusimamia, kulinda na kurejesha maliasili za majini na nchi kavu.

Mradi huu wenye lengo la kuhifadhi IKOLOJIA YA MAHALE kuwa endelevu katika maswala ya  Afya na Mazingira, unafanya kazi kwa mfumo wa Utangamano unaohusisha Watu,Afya na Mazingira yaani (Population, Health and Environment – PHE) kwa  kuwawezesha wananchi kufanya Shughuli za Kilimo na Uvuvi endelevu.

Vijiji 22  vilivyopo kando ya ziwa Tanganyika, wilayani uvinza, mkoani kigoma ,shughuli kubwa hapa ni kilimo na uvuvi lakini kabla ya mradi huu wa Tuungane kilimo na uvuvi viliendeshwa holela, havikuzingatia kanuni bora na uhifadhi huku uvuvi haramu nao ulitishia maisha  na ustawi.

Katika kijiji cha katumbi mzee Itembe Bakari anasimulia mwenendo wa biashara ya uvuvi ilivyokuwa ikiwika na kuifanya katumbi kuwa kituo cha biashara ya samaki kutoka mataifa mbalimbali lakini Biashara hiyo ikadorola kutokana na Uvuvi Haramu na kupotea kwa Samaki Ziwani.

Kwa sasa Beach Management Unity-BMU zimeanzishwa na hivyo kuwa mkombozi wa wavuvi kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika ambapo wavuvi wanafanya shughuli zao kwa kufuata taratibu na kanuni za uvuvi.

Utunzaji wa kumbukumbu umesaidia kudhibiti uvuvi haramu na kulinda mazalia ya samaki  kwa maslahi ya watanzania sasa mambo ni mwendo wa tablet tuu. MSHIKANA TEMBE ni katibu wa BMU katika kijiji cha Katumbi anaelezea kuwa BMU zimewasaidia kudhibiti uvuvi haramu na uharibufu wa mali za Bahari.

Serikali ya kijiji cha Katumbi inakiri kuanza kuona faida ya kilimo kinachozingatia utaalamu,matumizi bora ya ardhi na uvuvi endelevu kama ambavyo mwenyekiti mtendaji wakijiji cha Katumbi MTUNDA KITOPENI anavyoeleza katika makala hii kuwa imewasaidia kuboresha maisha ya wananchi wa Kijiji hicho na pia kulinda mazingira katika maeneo yao.

Mahitaji ya mwanadamu ni mtambuka, ndivyo ambavyo swala la uzazi wa Mpango halikuachwa nyuma katika Mradi huu ambapo mratibu wa Pathfinder International katika Mradi wa Tuungane Marcel Kato anaelezea kuwa wanatumia watoa huduma wa kijamii-CBD kuhakikisha elimu ya uzazi wa mpango inawafikia wakazi wa Vijiji vinavyozunguka Ziwa Voctoria.

Katika Zahanati ya katumbi watoa huduma ngazi ya jamii wanafanya kazi kubwa ya kutoa elimu ya uzazi wa mpango na wanaelezea kufanikiwa sana katika kazi hiyo hasa kutokana na mwitikio wa Jamii kutumia njia za uzazi wa Mapango.

Jamii kukubali mabadiliko mapya mara nyingi kuna changamoto hususani kubadili mfumo wa maisha kutoka katika kuharibu mazingira na uvuvi haramu na kufanya shughuli nyingine mbadala.

Katika Kijiji cha RUKOMA vimeundwa vikundi katika ngazi ya jamii vya kuweka na kukopa vijulikanavyo kama COCOBA, kikundi hiki kinaitwa UKAKAMAVU wanawake wanaelezea mabadiliko makubwa waliyoyapata kutokana na kuwa katika umoja na kujipatia mikopo inayowawezesha kufanya biashara na kufanikiwa kimaisha.

Mwisho.

Makala ya James Range/Lutengano Haonga