Rais John Magufuli amefanya uteuzi na kuwahamisha vituo vya kazi Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa na Wilaya, na pia amefanya uteuzi wa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mkuu wa Itifaki.
Wakurugenzi Watendaji walioteuliwa ni Ndaki Muhuli anayekua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Tawala wa wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Rehema Bwasi anakua Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, Sheillah Lukuba anakua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na kabla ya hapo alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es salaam, Mohamed Mavura anakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani ambapo awali alikuwa Afisa katika Makao Makuu ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Wengine walioteuliwa na Rais Magufuli ni Ezekiel Magehema anayekua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya ambapo kabla ya hapo alikua Afisa Tarafa wa Malangali mkoani Iringa, . Diana Zacharia yeye anakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama Mkoani Mara na kabla ya uteuzi huo Kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Tarafa wa Ukerewe Mkoani Mwanza, Hanji Godigodi anakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe na kabla ya uteuzi alikuwa Afisa Elimu Taaluma wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Magaro anakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora na kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Tarafa wa Msata Mkoani Pwani.
Hawa Mposi anakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro na alikua Afisa Tarafa wa Ifakara Mkoani Morogoro na
Godwin Chacha yeye anakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro ambapo kabla alikuwa Afisa Tarafa wa Maswa Mkoani Simiyu,
Wakurugenzi Watendaji waliohamishwa vituo vya kazi ni aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro anaenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Mkoani Singida na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani Advera Ndebabayo anaenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Dkt Wilson Charles kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Dkt Charles anachukua nafasi ya Athuman Kihamia ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Kanali Wilbert Ibuge kuwa Balozi na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kanali Ibuge anachukua nafasi ya Balozi Grace Martin ambaye atapangiwa majukumu mengine ya Kibalozi.
Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo hii Leo.
Wakati huo huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kepteni Mstaafu George Mkuchika amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya (DAS) wawili.
Kepteni Mstaafu Mkuchika amemteua Charangwa Selemani Makwiro kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Mkoani Dar es Salaam kuchukua nafasi ya Sheillah Lukuba ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.
Thomas Salala ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mtwara, ambapo Kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya hao unaanza hii leo.