Majeruhi wa mwendokasi atoka hospitalini

0
242

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imesema majeruhi pekee wa ajali ya basi la mwendokasi iliyotokea Februari 22 mwaka huu mkoani Dar es Salaam, Osam Milanzi ameruhusiwa kutoka Hospitalini baada ya afya yake kuimarika.

Meneja uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi amesema akiwa hospitalini hapo Milanzi alipata huduma za kibingwa katika kitengo cha dharura, ICU, HDU na wodi 2A.

Amesema alipokelewa akiwa ameumia maeneo ya kichwa, mguu wa kushoto, mkono na bega upande wa kulia, ambapo ataendelea na huduma kama mgonjwa wa nje na atarudi kliniki baada ya wiki mbili.

MOI imewashukuru waandishi wa habari waliotangaza habari za Osam
Milanzi
na Watanzania wote ambao wameshirikiana nao katika kumuombea mgonjwa huyo.