Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewahakikishia Watanzania kuwa kazi ya ujenzi wa Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) Mw 2115 inayofanyika katika eneo la bonde la mto Rufiji ni kazi ya uhakika na inakwenda kwa kasi kama ilivyopangwa.
Majaliwa ameyasema hayo leo Mei 14, 2020 alipokuwa kwenye ziara ya kukagua hatua za utekelezaji wa mradi.
“Nimetembelea eneo la mradi na kujionea shughuli zote zinazoendelea, Kazi inayofanyika ni ya uhakika huku matumaini ni makubwa ya kukamilisha mradi mapema kabla ya muda uliopangwa” Kassim Majaliwa.
Aidha, ameeleza kuridhishwa na hatua za utekelezaji ambazo mradi umefikiwa na kueleza kuwa mradi huo wa Julius Nyerere ni mradi mkubwa na wa kimkakati huku akiwapa pongezi TANESCO kwa usimamizi na Wakandarasi kwa kazi nzuri.
