Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Wafanyabiashara wadogo (Machinga), kuitumia vyema teknolojia ili kujifunza mbinu mbalimbali za kukua na hivyo kuweza kuuza huduma na biashara zao ndani na nje ya nchi.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa wito huo mkoani Dar es Salaam alipokuwa akifungua rasmi Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (DITF) maarufu Sabasaba.
Ameipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kufanikisha maonesho hayo pamoja na matumizi ya kidijitali yaliyotumika kutangaza biashara za Watanzania.
Aidha, Waziri Mkuu ametambua mchango na ushiriki wa wafanyabiashara wa kigeni kutoka takribani nchi 20.
Maonesho ya Sabasaba ya mwaka huu yana jumla ya washiriki 3500, kati yao 116 ni kampuni za kigeni.