Majaliwa : Fikisheni pikipiki kwa walengwa

0
121

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa muda wa siku tano kuanzia leo hadi tarehe 12 mwezi huu, wizara ya Kilimo iwe imeondoa pikipiki zote wizarani na kuzikabidhi kwa Wakurugenzi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo alipokagua ofisi za wizara ya Kilimo zilizopo Dodoma na kukuta pikipiki zilizotolewa kwa ajili ya maafisa ugani zikiendelea kuwepo.
 
“Hii haikubaliki, Wakurugenzi wote waandikiwe barua waje wazichukue, kama kuna ufungaji wa plate number utafanyika huko huko, Jumapili saa 10 jioni ziwe zimefika kwa wahusuka.” ameagiza Waziri Makuu
 
Aprili 4 mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan alizindua ugawaji wa vitendea kazi vilivyoandaliwa na wizara ya Kilimo kwa ajili ya maafisa ugani wote nchini, vifaa ambavyo ni pamoja na pikipiki.