Majaliwa amjulia hali Lowassa Afrika Kusini

0
147

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa anayeendelea na matibabu Afrika Kusini.

Akizungumza na wanafamilia kwa niaba ya Rais Samia, Waziri Mkuu amewasilisha salaam za pole kutoka kwa Rais na kusema Rais anafuatilia hali ya Lowassa kwa ukaribu na anamwombea afya njema.

Waziri Mkuu ametoa salamu hizo leo jijini Johannesburg, Afrika Kusini ambako alienda kumjulia hali ya Lowassa.

Kwa upande wake, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Regina Lowassa amemshukuru Rais kwa jinsi ambavyo amekuwa karibu na wanafamilia na namna ambavyo anafuatilia matibabu ya mpendwa wao.

Naye mtoto mkubwa wa Lowassa na Mbunge wa Monduli, Fredrick Lowassa amewashukuru Watanzania kwa maombi yao ya kumtakia afya njema baba yao.