Majaliwa akoshwa utendaji wa Jiji la Dodoma

0
237

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameweka jiwe la Msingi la ujenzi wa kituo cha Polisi cha Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma chenye hadhi ya Daraja A wakati akielekea kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru na awamu ya pili ya ujenzi wa majengo ya serikali.

Waziri Mkuu amepongeza hatua hiyo iliyofikiwa kwenye mradi huo unaogharimu milioni 948 na kuyataka majiji mengine nchini kuiga mfano wa viongozi wa jiji la Dodoma linalokuwa kwa kasi

Aidha, ametembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa kitega uchumi unaotekelezwa na jiji la Dodoma, mradi ambao unajengwa kwa awamu mbili ukigharimu kiasi cha shilingi bilioni 59.3 ikiwa ni jengo lenye maduka, hoteli, kumbi za mikutano na huduma za kibenki