Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameanza ziara ya kikazi ya siku saba mkoani Mtwara, ambapo miongoni mwa shughuli anazofanya ni kuzindua Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) katika manispaa ya Mtwara, Mikindani.
Aidha, kuanzia Julai 07, 2023 Waziri Mkuu atakagua, kuweka mawe ya msingi na pia atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika halmashauri zote Tisa za mkoa wa Mtwara.
Miradi hiyo atakayoitembelea na kukagua ni pamoja na jengo la wagonjwa wa nje katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara ya Ligula, chujio la maji eneo la Mangamba – mradi unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mtwara (MTUWASA), Hospitali ya Kanda ya Kusini ya Mitengo na Bandari ya Mtwara.
Pia atafanya mikutano ya hadhara na kuzungumza na Wananchi katika halmashauri za mkoa huo.