Mahakimu wapya watakiwa kujifunza TEHAMA

0
114

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mustapha Siyani amewataka mahakimu hao wapya kujifunza TEHAMA kadri ulimwengu unavyokwenda ili waweze kuwahudumia Wananchi ipasavyo kupitia Teknolojia

Akizungumza mara baada ya uapisho wa mahakimu hao katika Mahakama ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Jaji Siyani amesema mahakimu hao 20 ni kati ya watuma maombi 900 waliokuwa wameomba kazi, wamepatikana kwa njia ya TEHAMA.

Aidha, amewataka mahakimu hao kutenda haki kwenye mahakama za mwanzo ikiwa ni pamoja na kuhamasisha suluhu kwenye mashauri mbalimbali ili kujenga uhusiano mzuri na wananchi wanaowahudumia.

Pamoja na mambo na mengine, amewataka kujiepusha na aina zozote za rushwa kwani kazi walioiomba ni kwa ajili ya kutoa haki pasi na huba kwani uhakimu ni kiapo.

“Nuru ninazoziona ziendelee kutamalaki kwani uaminifu utawasaidia kusimamia haki, na wananchi watawapima kwa matendo yenu hivyo mjenge imani kwa wananchi na mahakama, “amesema Siyani.