Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeridhia maombi ya kuongeza kiapo cha ziada kwenye kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demeokrasia na Manedeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.
Ombi hilo limewasilishwa mahakamani hapo na Wakili Peter Kibatala ambaye anamwakilisha mshitakiwa Mbowe katika shauri hilo mbele ya Jaji John Mgeta.
Wakili Kibatala pia ameomba mahakama hiyo itoe samansi kwa mteja wake kuwepo mahakamani hapo shauri hilo litakapotajwa.
Hata hivyo upande wa jamhuri wenye jopo la mawakili saba ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Hangi Changa umesema hauna pingamizi na maombi hayo hivyo kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine kutajwa kwa shauri hilo.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili Jaji Mgeta ameahirisha shauri hilo hadi Agosti 30, 2021 kwa ajili ya kutajwa.