Mahakama Kuu yakataa ombi la kutengua uamuzi wa Spika

0
188

Mahakama Kuu imekataa ombi la aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),- Tundu Lissu, kufungua shauri la maombi kutengua uamuzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, -Job Ndugai, uliosababisha ubunge wake kukoma.

Mahakama hiyo imesema kuwa, Lissu hakupaswa kuwasilisha ombi hilo, bali alitakiwa kufungua kesi ya kupinga uchaguzi katika jimbo hilo la Singida Mashariki.

Imesema kuwa, kama ombi hilo litakubaliwa, itasaabisha ukiukwaji wa katiba, kwa kuwa italazimika kuwa na Wabunge wawili katika jimbo moja.