MAHAKAMA KUU DIVISHENI YA KAZI YAJA NA TOVUTI

0
202

Kuzinduliwa kwa tovuti ya Mahakama Kuu Disheni ya Kazi kutasadia kufikiwa maamuzi ya kesi mbalimbali zinazohusu migogoro ya kazi.

Hayo yamebanishwa mkoani Dar es Salaam na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mustapha Siyani, wakati wa hafla ya uzinduzi wa tovuti maalum ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi.

Pia amesisitiza matumizi ya lugha ya kiswahili kwenye tovuti hiyo, kama nyenzo itakayowasaidia wananchi kujua kinachoendelea mahakamani.

Pamoja na mambo mengine Jaji Kiongozi Siyani amezitaka mahakama zote nchini ziwe zimeingia kwenye matumizi ya TEHAMA ifikapo mwaka 2025, ili kupunguza kabisa matumizi ya karatasi.

Naye Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi Salma Maghimbi ameeleza kuwa tovuti hiyo imekuja wakati muafaka na kwamba itakuwa msaada mkubwa katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na wadau wengine wa mahakama wanaotafuta haki.