Magari yaanza kupita daraja la Kiyegea

0
242

Magari yameanza kupita kwa majaribio katika daraja lililovunjika la Kiyegea linalounganisha mkoa wa Morogoro na Dodoma, baada ya kufanyika kwa matengenezo ya awali.

Akizungumza na TBC kutoka katika eneo hilo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kuwa, wataendelea kupitisha magari machache machache hadi matengenezo yatakapokamilika.

Amesema katika majaribio hayo, wameweza kupitisha gari la hadi tani Ishirini, hali inayoashiria kuwa matengenezo hayo
yanaendelea vizuri.

Awali akikagua matengenezo katika eneo hilo, Waziri Mkuu Majaliwa aliagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, Katibu Mkuu wa wizara hiyo pamoja na Wahandisi wote wa TANROADS mkoa wa Morogoro na Dodoma wakutane kwenye eneo la tukio na kuhakikisha njia hiyo inafunguka.