Magari yaanza kupita daraja jipya Wami

0
486

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa ameruhusu magari kuanza kupita kwa mara ya kwanza katika daraja jipya la Wami.

Profesa Mbarawa amesema hayo alipofika katika daraja hilo ili kuruhusu magari kupita katika daraja hilo jipya ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 96 hadi sasa.

Daraja hilo jipya la Wami linatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Rais Samia Suluhu Hassan kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Ujenzi wa daraja hilo jipya la Wami lenye urefu wa mita 513.5 na barabara unganishi ya kilomita 3.8 ulianza mwaka 2018.