Fadhil Maganya amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa
Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na kuwashinda wagombea wengine saba.
Maganya amechaguliwa kwa kura 578 kati ya 835 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa Jumuiya hiyo ya wazazi ya CCM uliofanyika jijini Dodoma.
Amemshinda aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Dkt. Edmund Mdolwa ambaye amepata kura 64.
Matokeo hayo yametangazwa na
msimamizi wa uchaguzi huo Maalim Kombo Hassan usiku wa kuamkia hii leo, baada ya kura kuhesabu kwa zaidi ya saa saba.
Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Doto Iddi Mabrouk ametangazwa mshindi kwa kupata kura 530 kati ya 736 zilizopigwa, huku akiwashinda wagombea wengine wanne.