Mafuta yazidi kushuka bei

0
115


Bei za mafuta zimeshuka kuanzia hii leo, ambapo kwa mkoa wa Dar es Salaam petroli itauzwa shilingi 2,886 kwa lita, dizeli shilingi 3,083 na mafuta ya taa shilingi 3,275 kwa lita.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema
kushuka kwa bei za mafuta kumetokana na kushuka kwa bei ya bidhaa hizo katika soko la dunia kwa mwezi Agosti mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa ya EWURA,
iliyotolewa kwa vyombo vya habari, bei hizo katika soko la dunia ndizo zimetumika katika kukokotoa bei za mafuta za hapa nchini kwa mwezi huu wa Oktoba ambazo zimepungua kwa asilimia 7.4, 3.9 na 1.9 kwa mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa.