Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kupanda kwa bei kikomo za bidhaa za mafuta, zilizoanza kutumika Leo Septemba 06, 2023.
Kwa mujibu wa EWURA, bei za rejareja za petroli katika mkoa wa Dar es Salaam ni shilingi 3,213 kwa lita moja, dizeli shilingi 3,259 na mafuta ya taa ni shilingi 2, 943 kwa lita moja.
EWURA imesema mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Septemba 2023 yanayoonesha kupanda kwa bei yanatokana na kupanda kwa gharama za mafuta katika soko la dunia kwa hadi asilimia 21, gharama za uagizaji wa mafuta hadi asilimia 62 ikilinganishwa na mwezi Agosti 2023 na maamuzi ya kisiasa katika nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi (OPEC+).
Bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini kwa mwezi uliopita zilizoanza kutumika kuanzia Agosti 02, 2023, bei za rejareja za mafuta katika mkoa wa Dar es Salaam petroli ilikuwa shilingi 3,,199 kwa lita moja, dizeli shilingi 2,935 na mafuta ya taa shilinhi 2,668 kwa lita moja.