Mafuriko yaleta maafa Mtwara

0
173

Mtu mmoja amefariki dunia baada ya kusombwa na maji mkoani Mtwara, kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani humo.

Kufuatia mvua hizo, .mkuu wa mkoa wa Mtwara, – Gelasius Byakanwa amewataka Wakazi wanaoishi kwenye maeneo hatarishi na mabondeni kuhamia kwenye maeneo ambayo yametengwa.

Byakanwa amesema hayo wakati akifungua kikao cha kawaida cha bodi ya barabara na kusema kuwa, Wanafunzi wengi hawajaweza kuanza shule tangu zifumguliwe kutokana na maeneo wanayoishi kukumbwa na mafuriko

Ameuagiza uongozi wa Wakala wa Brabara za Mijini na Vijijini (TARURA) mkoani Mtwara kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kiangalia namna ya kukarabari barabara zilizoharibiwa na mvua ili ziweze kupitika.