Mafanikio ya ziara ya Rais nchini China na Misri

0
110

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, amezungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Rais Samia nchini China na Misri.

Zuhura amesema ziara za Rais zimekuwa na manufaa makubwa ambapo nchini China alifanya mazungumzo na Rais Xi Jinping katika kushirikiana kwenye masuala mbalimbali.

Miongoni mwa hayo ni kushirikiana kiuchumi ambapo sasa Tanzania itaanza kuuza parachichi nchini China pamoja na mabondo.

Pia wamekubaliana kutotoza ushuru kwa 98% kwa bidhaa kutoka Tanzania kwenda China, kukuza uchumi wa kidijitali, uchumi wa buluu na kushirikiana katika mradi wa kufufua reli ya TAZARA.

Zuhura amesema Rais akiwa nchini Misri kushiriki mkutano wa COP27, alipata fursa ya kukutana na baadhi ya marais kujadili nishati ya umeme ambapo Benki ya Dunia imekubali kutoa dola bilioni 18 katika uwekezaji wa nishati jadidifu.

Mwaka 2024 Tanzania na China zitatimiza miaka 60 ya ushirikiano na hivyo kukubaliana kutumia diplomasia kukuza  zaidi sekta ya utalii.