Maendeleo makubwa miaka 59 ya Mapinduzi

0
135

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), Profesa Mohamed Makame Hajji amesema hatua kubwa ya maendeleo imepigwa katika miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Profesa Makame ametoa kauli hiyo wakati wa mahojiano maalum na TBC katika kipindi cha Jambo Tanzania ambapo ameelezea mafanikio yanaonekaza zaidi katika nyanja za elimu na uchumi.

Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya nane pekee imefanya mageuzi makubwa katika elimu hasa katika maboresho ya miundombinu na nyenzo za kufundishia wanafunzi.

Profesa Makame amesema tayari maboresho ya sekta ya elimu yameanza kufanyika na ndio maana miundombinu ya kufundishia imeboreshwa na baada ya muda mfupi matokeo yataanza kuonekana.

Kuhusu uchumi, amesema, falsafa ya uchumi wa buluu inakuja kutafsiri namna bora ya kutumia rasilimali za bahari katika kuwaletea maendeleo wananchi wa visiwa hivyo.