MAELEKEZO YA RAIS SAMIA KWA OFISI YA WAZIRI MKUU SIKU YA MASHUJAA

0
136

Rais Samia Suluhu Hassan ameielekeza ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na wahusika wengine kuendelea kusimamia kwa karibu ujenzi wa Mnara na Uwanja wa Mashujaa uliopo mkoani Dodoma pamoja na miundombinu mingine, ili ikamilike kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa.

Ametoa maelekezo hayo alipokuwa akihutubia Taifa katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa uliopo ndani ya Mji wa Serikali Dodoma.

Rais Samia ameitaka wizara ya Fedha kuhakikisha inatoa fedha kwa kuzingatia mpango kazi wa ujenzi huo na kusiwepo na ucheleweshwaji wowote.

Aidha, Rais Samia ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuwaenzi Mashujaa kwa kudumisha amani, umoja, mshikamano na utulivu wa Taifa la Tanzania huku akisisitiza kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya nchi.