Maduka ya dawa ndani ya mita 500 za hospitali kuondolewa

0
227

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa hadi Julai Mosi mwaka huu maduka yote binafsi yaliyojengwa ndani umbali wa mita 500 kutoka hospitali ilipo, yawe yameondolewa kwani uwepo wake ni kinyume na kanuni.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili na kueleza kuwa sheria inazuia mduka kujengwa karibu na hospitali.

“Maduka ya dawa yote ndani ya Mita 500 nje ya Hospitali yapo kinyume cha sheria kwasababu Hospitali dawa hakuna lakini kwanini maduka ya nje dawa zipo haikubaliki,” amesema Waziri.

Aidha, amesema kwamba serikali inakwend kuboresha huduma za afya katika Hospitali za Rufaa za Kanda ili inapotokea mgonjwa amepewa rufaa kwenda Muhimbili, iwe ni kwa tatizo lililoshindikana.

“Mama Samia (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ameshanielekeza, na tunakwenda kuboresha huduma kwenye Hospitali za Rufaa za Kanda na Mikoa na Hospitali za Halmshauri ili Mtu akija Muhimbili aje na jambo ambalo limeshindikana kule chini. Tumeona hapa Hospitali za Mwananyamala na Temeke zinaleta Wagonjwa Muhimbili eti kwa sababu hawana damu huo ni uzembe hatuwezi kuukubali,” amesisitiza.