Madiwani wa Halmashauri ya Meru mkoani Arusha, wamelalamikia migogoro ya mipaka kati ya wilaya hiyo na wilaya ya Arusha ambayo imekuwa ikiikosesha mapato kutokana na maafisa kutoka wilaya ya Arusha kukusanya mapato yatokanayo na mashamba makubwa ya maua yaliyopo Meru.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo, Mwenyekiti Msaidizi wa Halmashauri ya Meru, Nelson Mafie amesema ni vema wataalamu wakapima maeneo hayo ili kubaini mipaka.
