Madiwani wakerwa na wajawazito kujifungulia mapokezi, watoa maagizo

0
397

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge wamewaagiza Afisa Utumishi na Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) kuwachukua hatua Wauguzi wote walisababishia baadhi ya wakinamama kujifungulia mapokezi wakiwa wanasubiri huduma.

Azimio hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la Sikonge la kujadili na kupitia mapendekezo ya makisio ya mapato na matumizi ya mwaka 2020/21 baada ya baadhi ya Madiwani kulalamikia uzembe wa wauguzi ulisababisha baadhi ya wanawake kujifungua bila msaada wa Muunguzi.

Baraza hilo limesema kuwa litawachukulia hatua Afisa Utumishi na Mganga Mkuu wa Wilaya endapo watashindwa kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria ya watumishi waliochini yao.

Awali Diwani wa Kata ya Kipanga, Upendo Mgombozi alisema mama mmoja mjamzito alilazimika kujifungulia mapokezi baada ya muuguzi wa zamu kudai hawezi kwenda kumsaidia kwa sababu ya hali aliyonayo kiafya. 3Mama huyo alijifungua mbele ya mume wake akiwa hana msaada na kuongeza kuwa angaweza hata kupoteza maisha kwa sababu ya kutokuwa na msaada wa mtaalamu.

Akijibu hoja za madiwani Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Dkt. Peter Songoro alisema baadhi ya wauguzi waliozembea na kusababisha baadhi ya wanawake kujifungia wakiwa wanagonja huduma wameshapewa onyo na muuguzi mwingine tuhuma zake zinaendelea kufanyiwa kazi na itakapokamilika watatoa taarifa ya hatua waliyomchukulia.