MADEREVA watakaobeba viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika (SADC) wameaswa kuwa na weledi wakati wa kuwaendesha viongozi hao.
Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Amani wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda Stephen Mbundi ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo kwa madereva watakaosafirisha viongozi wa SADC yaliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) jijini Dar es Salaam.
Mbundi amesema mkutano huo ni wa kimataifa Dunia nzima inaangalia hivyo kama nchi haitaki aibu yeyote katika ujio wa viongozi hao ikiwa ni pamoja na kuwa na lugha nzuri katika mawasiliano.
Amesema nchi imewapa heshima madereva katika mkutano huo na kuandika historia
kwa nchi katika utoaji wa huduma ya kuwasafirisha na kuongeza kuwa masilahi yao
yatalindwa.
Mratibu wa Mafunzo hayo ni Mkaguzi Msaidizi Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama
Barabarani Ibrahim Samwix.
Nae Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)Profesa Zakaria Mganilwa
amesema kuwa mafunzo hayo ni faida kwa madereva katika mkutano wa SADC.
Amesema kuwa madereva waliopata mafunzo wa uzoefu kilichofanyika ni kuwaongezea maarifa namna kuwa na weledi katika kuwaendesha viongozi wa SADC.