Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam limewatahadharisha madereva wanaotumia vyombo vya moto kuacha mara moja kutumia barabara za mabasi ya mwendo kasi ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.
Tahadhari hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Lazaro Mambosasa baada ya jeshi hilo kuwashikilia madereva wa pikipiki 20 kwa tuhuma za kulishambulia basi la mwendokasi na kusababisha uharibifu.
Kamanda Mambosasa pia amesema jeshi hilo linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukutwa na vipande 20 vya meno ya tembo vyenye thamani ya shilingi Milioni 87.