Madereva wa Bodaboda hatarini kuugua ugonjwa wa Moyo

0
198

Madereva pikipiki maarufu Bodaboda wako hatarini kuugua magonjwa ya
mfumo wa upumuaji ambayo yanaweza kusababisha kupata ugonjwa wa moyo.

Akizungumza mkoani Kigoma, Mganga Mkuu wa mkoa huo Dkt, Paul Chaote amewataja madereva hao ni wale ambao hawavai kofia ngumu, na vifaa vinginge vya  kukinga Kifua na mgongo.

Dkt.Chaote amesema madhara hayo si ya moja kwa moja bali yanatokea
baada ya kupita kipindi kirefu  kwa  madereva wa aina hiyo.