Madarasa mapya yazinduliwa Kusini Unguja

0
88

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua vyumba sita vya madarasa katika shule ya msingi Muyuni, ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kuzindua miradi ya maendeleo kuelekea kilele cha Tamasha la watu wa Kizimkazi.

Mbali na vyumba hivyo vya madarasa, Rais Samia pia amezindua darasa kwa ajili ya mitihani na ukumbi wa Jumuiya ya watu wa Muyuni kwenye shule ya sekondari ya Muyuni wilaya ya Kusini Unguja.

Akizungumza mara baada ya kuzindua miradi hiyo Rais Samia amesema anajisikia faraja kuona anachangia maendeleo ya mahali alipozaliwa miaka 63 iliyopita.

Amewataka Wananchi wa Muyuni kutunza miundombinu hiyo ili iwasaidie kwa muda mrefu.