Mabalozi watano wawasilisha hati za utambulisho

0
319

Rais Samia Suluhu Hassan leo amepokea hati za utambulisho za Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi waliowasilisha kwa nyakati tofauti hati zao za utambulisho kwa Rais Samia Suluhu Hassan wanatoka katika nchi za Namibia, Msumbiji, Uturuki, Italia na Ireland.

Tukio la Rais Samia Suluhu Hassan kupokea hati hizo za utambulisho kutoka kwa Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini limefanyika Ikulu jijini Dar es salaam, na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula.

Baada ya kupokea hati hizo za utambulisho, Rais Samia Suluhu Hassan kwa nyakati tofauti amefanya mazungumzo na Mabalozi hao.