Mabalozi Watano wawasilisha hati za utambulisho

0
263

Rais John Magufuli leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi Watano wataoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Rais Magufuli amepokea hati hizo Ikulu jijini Dar es salaam kutoka kwa Mabaloziwapya wa India,Zimbabwe,Angola, Denmark na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kiarabu ya Saharawi.

Mabalozi hao ni Mahayub Buyema Mahafud wa Saharawi, Sanjiv Kohil wa Indiana Meja Jenerali Anselem Nhamo Sanyatwe kutoka nchini Zimbabwe.

Wengine ni Balozi Sandro Renato Agostinho De Oliveira kutoka Angola na Mette Norgaard Dissing Spandet wa Denmark.