Mabalozi wanne wapangiwa vituo vya kazi

0
267

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Ali Idd Siwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Balozi Siwa ameteuliwa kwa kipindi cha pili kushika nafasi hiyo baada ya muda wa Bodi hiyo kuisha tarehe 21 Septemba, 2021.

Uteuzi huo umeanza tarehe 7 Desemba, 2021.

Aidha, Rais Samia amewapangia vituo vya kazi Mabalozi wafauatao:-

⦁ Balozi Said Shaib Mussa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait.
⦁ Balozi Fredrick Ibrahim Kibuta kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi.
⦁ Balozi Said Juma Mshana kuwa Balozi wa Tanzania Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
⦁ Balozi Alex Gabriel Kalua kuwa Balozi wa Tanzania katika Taifa la Isarael.