Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekutana kwa nyakati tofauti na kufanya mazungumzo na Balozi wa Denmark nchini Mette Spandet, Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier na Balozi wa Qatar nchini Abdulla Jassim Al -Maadadi.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam, Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier amemueleza Makamu wa Rais kuhusu mipango na malengo ya maendeleo ya nchi yake nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na kuendeleza na kukuza ushirikiano kati ya nchi hizo.
Kwa upande wake Balozi wa Denmark nchini, -Mette Spandet aliyefika kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kujitambulisha, amemuhakikishia kuwa nchi yake itaendelea kudumisha utamaduni uliojengwa na nchi hizo Mbili wa kushirikiana katika kuendeleza Uchumi wa Viwanda.
Aidha Makamu wa Rais amemtakia heri Balozi wa Qatar nchini,-Abdulla Jassim Al -Maadadi baada ya kumaliza muda wake wa kufanyakazi nchini, na amemuahidi kuwa Tanzanua itaendelea kudumisha ushirikiano na Qatar.