Mabalozi tisa waliowasilisha hati za utambulisho Ikulu leo

0
238

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amepoea hati za utambulisho wa ubalozi kutoka kwa mabalozi wateule tisa walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi waliowasilisha hati zao za utambulisho ni;

  1. Maria Amelia Mario De Paiva, Balozi mteule wa Ureno nchini mwenye makazi yake nchini Msumbiji
  2. Douglas Foo Peow Yong, Balozi mteule wa Singapore nchini mwenye makazi yake nchini Singapore
  3. Alex G. Chua, Balozi mteule wa Ufilipino nchini mwenye makazi yake nchini Kenya
  4. Angela Veronica Comfort, Balozi mteule wa Jamaica nchini mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini
  5. Dkt. Christian Fellner, Balozi mteule wa Austria nchini mwenye makazi yake nchini Kenya
  6. Fransisca Ashiete Odunton, Balozi mteule wa Ghana nchini mwenye makazi yake nchini Kenya
  7. Jesus Agustin Manzanila Puppo, Balozi mteule wa Venezuela nchini mwenye makazi yake nchini Kenya
  8. Yacin elmi Bouh, Balozi mteule wa Djibouti nchini mwenye makazi yake nchini Kenya
  9. Oded Joseph, Balozi mteule wa Israel nchini mwenye makazi yake nchini Kenya

Hafla hiyo inafanyika Ikulu Jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2020.