Mabalozi 6 wawasilisha hati za utambulisho

0
153

Rais Samia Suluhu Hassan leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi sita wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi waliowasilisha hati hizo Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma ni pamoja na Jorge Sánches ambaye ni Balozi Mteule wa Hispania nchini na Kyle Michael Nunas, Balozi mteule wa Canada nchini.

Wengine ni Balozi mteule wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo nchini
Jean -Pierre Kassala na Balozi wa Finland nchini Tereza Zitting.

Balozi Mteule wa Sudan Kusini nchini, Loyang Johnson Okot Jekery na Balozi Mteule wa Iran nchini Hossein Alvand Behineh nao ni miongoni mwa mabalozi sita waliowasilisha hati zao za utambulisho kwa Rais Samia Suluhu Hassan.