Maandalizi ya wiki ya Nenda kwa Usalama

0
160

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Adam Malima akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya kitaifa ya Baraza la Usalama Barabarani, amekagua maeneo mbalimbali utakapofanyika ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Kitaifa.

Mwaka huu wiki ya
Nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa inafanyika mkoani Mwanza ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Mara baada ya kukagua maeneo mbalimbali ya maandalizi ya wiki hiyo ikiwemo vyombo vya moto, Malima ameonesha kuridhishwa na namna wadau walivyojipanga kutoa elimu na mafunzo kwa wananchi na watumiaji wa vyombo vya moto.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Wilbard Mutafungwa amesema wadau wote muhimu wa masuala ya usalama barabarani wameshirikishwa wakiwemo watumiaji wa barabara.