Maandalizi ya Kongamano la wafanyabiashara wa Uingereza yashika kasi

0
260

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Latifa Khamis ameongoza kikao cha pili cha maandalizi ya Kongamano la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Uingereza kilichofanyika leo tarehe 1 Septemba, 2021 Mkoani Dar es Salaam.

Lengo la Kongamano hilo ni kuimarisha uhusiano wa kibiashara uliopo, kuanzisha uhusiano mpya, kujadili fursa za biashara na uwekezaji , kutatua vikwazo vya kibiashara na uwezeshwaji wa kifedha katika miradi inayoendelea kutekelezwa na nchi hizi mbili.

Kongamano hili linatarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Novemba, 2021 na kushirikisha Wadau takribani 200 kutoka sekta ya Kilimo, Madini, Nishati na Miundombinu kutoka nchini Uingereza na Tanzania linaratibiwa na TanTrade kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Viwanda na Biashara, Ubalozi wa Uingereza Nchini Tanzania na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF)